Swali: Mwenye kusema kuwa Ashaa´irah hawana isipokuwa vijimakosa fulani katika baadhi ya sifa za Allaah maneno yake ni sahihi?
Jibu: Sifa nyingi wanazikanusha na hawathibitishi isipokuwa saba tu na wengine wanathibitisha sifa kumi na nne tu. Vipi mtu atasema wana vijimakosa vidogo tu ilihali wanapinga sifa za Allaah (´Azza wa Jall)? Isitoshe jengine ni kwamba hawategemei dalili za Kishari´ah katika ´Aqiydah. Wanategemea kanuni za kimantiki na elimu ya falsafa. Wanategemea elimu ya mantiki na falsafa na hawategemei Qur-aan na Sunnah. Vipi mtu anaweza kusema kuwa hawana isipokuwa vijimakosa vidogo tu? Huyu ima hajui hali yao au anataka kuwapaka watu mchanga wa machoni.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (28) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2140
- Imechapishwa: 12/07/2020
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)