Arudi swalah tena kwa aliyeswali kwa Tayammum kutokana na baridi kali?

Swali: Ni lazima kwake kuoga josho la janaba baridi ikiondoka asubuhi?

Jibu: Hapana, hatoirudia. Ataoga peke yake. Hadiyth inasema:

“Udongo ni wudhuu´ wa muislamu hata kama hatopata maji kwa miaka kumi. Akipata maji, basi na amche Allaah na ayafikishe kwenye ngozi yake.”

Swali: Kwa hiyo si lazima kwake kuoga?

Jibu: Ni lazima kwake kuoga kutokana na janaba. Kuhusu kutia wudhuu´ tena upya, hapana ameshatawadha. Ikiwa aliswali, basi swalah yake ni sahihi na hapaswi kurudia chochote. Lakini ataoga kwa ajili ya janaba peke yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24764/هل-يلزم-من-تيمم-لشدة-البرد-الغسل-لاحقا
  • Imechapishwa: 07/12/2024