ar-Raajhiy kuhusu kususa bidhaa za Denimark

Swali: Ni upi usahihi wa Fatwa inayonasibishwa kwako kuhusu kuendelea kususa mashirika ya bidhaa za Denimark na unashauri nini kuhusiana na wao na kukomeka na ususaji?

Jibu: Ndio, ni kweli. Nilitoa Fatwa kwa ushirikiano wa Shaykh ´Abdullaah bin Jibriyn na Shaykh ´Abdur-Rahmaan al-Barraak juu ya ususaji na kwamba ni wajibu kuendelea kuwasusa. Makafiri hawa waliomtukana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) lililokuwa la wajibu ni kuwaua na kuwachukulia hatua. Hatuna njia nyingine zaidi ya kuwasusa. Ususaji hautosita mpaka watu hawa wajisalimishe kwa Waislamu na wasimamishiwe adhabu ya Allaah. Maadamu hawajajisalimisha, ususaji bado utaendelea. Hatuna njia nyingine zaidi ya hii. Ikiwa hatuwezi kuwasimamishia adhabu tunaweza kuwasusa. Kuwasusa ndio kunaweza kukawaathiri. Maneno tu hayawaathiri lolote. Lakini ususaji umewaathiri hivi sasa na uchumi wao na hilo limewafanya wao kulalamika. Ni wajibu kuendelea kuwasusa.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=4734
  • Imechapishwa: 01/05/2015