Swali: Wakati ´Iysaa (´alayhis-Swalaatu was-Salaam) ataposhuka atakuwa na ´Aqiydah yake ya zamani au ´Aqiydah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: ´Aqiydah ya Mitume ni moja. Hakuna tofauti kati ya Mitume inapokuja katika ´Aqiydah. ´Aqiydah yao ni Tawhiyd na hakuna tofauti juu ya hilo.

Ama Shari´ah ambayo ni inahusiana na hukumu, ´Iysaa atahukumu kwa Shari´ah ya Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Atakuwa ni mwenye kumfuata Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14340106.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015