Anayowahi mswaliji aliyechelewa yanazingatiwa ndio ya kwanza au ya mwisho?

Swali: Yale anayowahi yule anayejiunga na imamu yanazingatiwa ni ya kwanza au ya mwisho?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba yale anayowahi katika swalah yanazingatiwa ndio ya kwanza na yale anayoyakidhi yanazingatiwa ndio ya mwisho. Akiwahi Rak´ah mbili za mwisho za Dhuhr na akaweza  kusoma al-Faatihah na Suurah nyengine pamoja na imamu afanye hivo. Imamu akitoa Tasliym na yeye akasimama kukamilisha yaliyompita akomekee katika al-Faatihah peke yake. Kwa sababu yale anayolipa yanazingatiwa ndio ya mwisho katika swalah yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Swalini yale mnayoyadiriki na kamilishe yale yaliyokupiteni.”[1]

[1] al-Bukhaariy na Muslim.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/448)