Anayelipa Fajr baada ya jua kuchomoza anasoma kwa sauti ya juu au kimyakimya?

Swali: Muislamu akilazimika kuswali Fajr kwa kulipa baada ya jua kuchomoza, je, aiswali kwa sauti ya juu au kimyakimya? Je, ataswali Sunnah ya Fajr kabla yake au baada yake?

Jibu: Aliyepitwa na swalah katika wakati wake, kwa maana swalah ya Fajr, anaswali kwa sauti ya juu. Pia anatakiwa kuanza na Sunnah ya Raatibah. Hivi ndivyo alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipolala na kupitwa na swalah ya Fajr katika baadhi ya safari zake. Aliiswali kama alivyokuwa akiiswali katika wakati wake kwa adhaana na Iqaamah, kisha akaswali Sunnah ya Raatibah, halafu akaswali swalah ya faradhi. Hivyo ndivyo ilivyowekwa katika Shari´ah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/349)
  • Imechapishwa: 14/03/2026