Anayejitwahirisha na hedhi kufumua nywele zake

Swali: Je, ni lazima kwa mwanamke kufumua nywele zake wakati wa kujitwahirisha na hedhi?

Jibu: Hapana, inapendeza tu. Kwa ajili hiyo imekuja katika Hadiyth ya Umm Salamah iliyopokelewa na Muslim ambaye aliuliza:

“Je, nizifungue ninapotoka kwenye hedhi?” Akamjibu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Hapana. Hapana vyenginevyo inakutosha kuzimiminia maji.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24761/حكم-نقض-الشعر-لغسل-الحيض
  • Imechapishwa: 07/12/2024