1964- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Huu ndio mwaminifu wa Ummah huu.”

Ameipokea Muslim, al-Haakim, Ahmad na Abu Ya´laa kupitia njia nyingi kutoka kwa Hammaad bin Salamah, kutoka kwa Thaabit, kutoka kwa Anas ambaye amesema:

“Watu wa Yemeni walikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakasema: “Tuagizie mtu ambaye atatufunza Sunnah na Uislamu.” Akaushika mkono wa Abu ´Ubaydah na akasema: “Huu ndio mwaminifu wa Ummah huu.”

Katika Hadiyth kuna faida kubwa, nayo ni kwamba maelezo ya mtu mmoja (خبر الآحاد) ni hoja katika mambo ya ´Aqiydah, kama ambavo ni hoja vilevile katika mambo ya hukumu. Kwa sababu tunajua kwa yakini kabisa kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumtuma Abu ´Ubaydah Yemen ili awafunze mambo ya hukumu peke yake, bali pia mambo ya ´Aqiydah. Lau ingelikuwa maelezo yenye kutoka kwa mtu mmoja hayafidishi elimu ya kidini katika mambo ya ´Aqiydah na wala hayasimamishi hoja, basi kutumilizwa kwa Abu ´Ubaydah peke yake awafunzee ingelikuwa ni upuuzi, jambo ambalo Shari´ah imetakasika nalo. Kwa hivyo inathibitisha kiyakini kabisa kwamba maelezo yanayotoka kwa mtu mmoja ni yenye kufidisha elimu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (4/605)
  • Imechapishwa: 05/08/2020