Swali: Akitwahirika mwanamke mwenye hedhi wakati wa ´Aswr au ´Ishaa aswali pamoja nazo Dhuhr na Maghrib kwa kuzingatia kwamba zinakusanywa pamoja?

Jibu: Mwanamke akisafika kutokamana na hedhi na damu ya uzazi wakati wa ´Aswr basi analazimika kuswali Dhuhr na ´Aswr pamoja kutokana na maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Kwa sababu wakati wake ni mmoja kwa yule mwenye udhuru kama mfano mgonjwa na msafiri. Yeye pia ni mwenye udhuru kwa sababu ya kuchelewa kusafika kwake. Vivyo hivyo akitwahirika wakati wa ´Ishaa basi kutamlazimu kuswali Maghrib na ´Ishaa pamoja kama ilivyotangulia. Jopo la Maswahabah (Radhiya Allaahu ´anhum) wamefutu hivyo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (10/217)
  • Imechapishwa: 05/09/2021