Swali: Kipindi cha mwisho kuna bwana mmoja amejitokeza na kusema kuwa anataka kuunda madhehebu mapya katika Fiqh. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Haya ni maneno mabovu ambayo yanatakiwa kupuuzwa. Nadhani kuwa hayahitaji hata kuraddiwa. Inatosha kwamba anajiona mwenyewe kuwa ni miongoni mwa wanazuoni wakubwa na anasema kuwa ndugu zangu wanazuoni pengine wasinikubalie juu ya hilo. Pili ni kwamba haoni kuwa Hadiyth zilizosimuliwa na msimulizi mmoja hazitakiwi kufanyiwa kazi ingawa zitakuwa zimethibiti, kama wanavyoona Mu´tazilah na baadhi ya Mashaykh wenye kasumba. Tatu ni kwamba maneno yake haya yanaleta hisia fulani ya kujikuza na kujikweza. Allaah amrehemu mtu ambaye anajua kiwango chake. Namshauri ndugu huyu arejee kwa Allaah na atubu kwa Allaah kutokana na aliyoyasema. Tunamuombea kwa Allaah amwongoze, amuwafikishe, amrekebishe na amrejeshe katika haki.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin Sa´d as-Suhaymiy
  • Mfasiri: Firqatunnaja.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=gyMnFmQ6Cmg&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 19/09/2023