Anataka kutumia mali aliyopewa aitoe swadaqah

Swali: Mmoja wa wafanyao hisani amenipa mali ili nitoe swadaqah kwa niaba yake. Je, inafaa kwangu kuichukua mali hiyo badala ya mtu mwenye dhiki ambaye ana madeni na hawezi kuyatekeleza?

Jibu: Huna ruhusa kufanya hivyo. Bali unatakiwa kuitumia kwa namna ambayo aliyetoa swadaqah amekuwakilisha kufanya hivyo, kwa sababu kufanya hivyo kuna maslahi yako binafsi.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
  • Imechapishwa: 19/09/2026