Swali: Ni ipi hekima ya kufunga siku za jumatatu na alkhamisi?

Jibu: Kwa sababu ni siku mbili ambazo matendo huwasilishwa kwa Allaah, kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoulizwa kuhusu kufunga siku hizo:

”Hakika ni siku mbili ambazo matendo huwasilishwa kwa Allaah. Hivyo basi napenda matendo yangu yawasilishwe nikiwa nimefunga.”

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
  • Imechapishwa: 19/09/2026