Swali: Bibi yangu alinibeba nikiwa na miezi minne ambapo akanilisha maziwa ya kopo. Nilipolia alikuwa akinipa titi lake ili kunyamaza na kunituliza ilihali kipindi hicho ni mzee na ana umri wa miaka sitini na hakuwa na maziwa na mume wake alifariki miaka ishirini iliyopita. Je, inajuzu mimi kumuoa msichana wa ami yangu, ndugu wa baba yangu?
Jibu: Ndiyo, ikiwa bibi hakukunyonyesha, bali alikuwa anakunywesha maziwa ya kopo na anakupa titi lake kwa ajili ya kukutuliza na kukubembeleza tu, bila ya kutoa maziwa, basi hilo halidhuru na hakuna tatizo. Inajuzu. Ama ikiwa alikunyonyesha – hata kama ni mzee – ikiwa alitoa maziwa na akakunyonyesha unyonyeshaji kamili wa mara zisizopungua tano, basi anakuwa mama yako (ikiwa ni mama wa baba yako) na wewe unakuwa ndugu wa baba yako, ndugu wa ami zako na mjomba kwa watoto wao. Lakini muda wa kuwa hakutoa maziwa, bali alikuwa anakubembeleza kwa kukupa titi lake bila maziwa, basi hilo halina madhara.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3265/حكم-الرضاع-ممن-انقطع-لبنها-والزواج-من-ابنة-العم
- Imechapishwa: 06/08/2026
Swali: Bibi yangu alinibeba nikiwa na miezi minne ambapo akanilisha maziwa ya kopo. Nilipolia alikuwa akinipa titi lake ili kunyamaza na kunituliza ilihali kipindi hicho ni mzee na ana umri wa miaka sitini na hakuwa na maziwa na mume wake alifariki miaka ishirini iliyopita. Je, inajuzu mimi kumuoa msichana wa ami yangu, ndugu wa baba yangu?
Jibu: Ndiyo, ikiwa bibi hakukunyonyesha, bali alikuwa anakunywesha maziwa ya kopo na anakupa titi lake kwa ajili ya kukutuliza na kukubembeleza tu, bila ya kutoa maziwa, basi hilo halidhuru na hakuna tatizo. Inajuzu. Ama ikiwa alikunyonyesha – hata kama ni mzee – ikiwa alitoa maziwa na akakunyonyesha unyonyeshaji kamili wa mara zisizopungua tano, basi anakuwa mama yako (ikiwa ni mama wa baba yako) na wewe unakuwa ndugu wa baba yako, ndugu wa ami zako na mjomba kwa watoto wao. Lakini muda wa kuwa hakutoa maziwa, bali alikuwa anakubembeleza kwa kukupa titi lake bila maziwa, basi hilo halina madhara.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3265/حكم-الرضاع-ممن-انقطع-لبنها-والزواج-من-ابنة-العم
Imechapishwa: 06/08/2026
https://firqatunnajia.com/anataka-kumuoa-binamu-yake-baada-ya-kunyonyeshwa-na-bibi-yake/