Anaenda mara nyingi kwa daktari na kumfunulia uso lakini hatumii dawa anazoelekezwa

Swali: Huenda hospitalini mara nyingi na humfunulia uso wangu daktari. Lakini situmii dawa anayonipa. Je, nina dhambi?

Jibu: Haijuzu kwake kwenda kwa daktari na akafunua uso mbele yake. Midhali humweleza dawa na haitumii, faida iko wapi? Lakini akiwa na haja ya kweli hakuna neno akamfunulia uso wake daktari juu ya yale anayohitajia kutazama. Kwa sharti asiwe naye faragha. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwanaume asikae faragha na mwanamke isipokuwa awe pamoja naye Mahram.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (68) http://binothaimeen.net/content/1536
  • Imechapishwa: 17/02/2020