Swali: Ni ipi hukumu ya kusikiliza Anaashiyd za Kiislamu zinazoambatana na kupigwa dufu kwa lengo la kuwavutia vijana kwazo na ili wasisikilize nyimbo chafu?

Jibu: Kusikiliza Anaashiyd njema zinazohimiza jihaad, ukarimu na kutoa na mashairi mazuri, hakuna tatizo kwayo. Lakini sharti zisiwe na dufu, ngoma wala chombo chochote cha muziki. Ama zikisindikizwa na ngoma, dufu, ala ya muziki ya udi, kinubi au rababa, basi zinakuwa ni haramu. Lazima ziwe tupu na zisizo na kitu chochote. Anaashiyd zilizo njema kuhusu jihaad, maadili mema, kuwafanyia wema wazazi na katika kuunga undugu wa jamaa, lakini bila kuandamana na dufu, ngoma, kinubi, rababa wala chombo chochote cha muziki.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2442/سماع-الاناشيد-الاسلامية-التي-يصاحبها-دف
  • Imechapishwa: 29/03/2026