an-Nawawiy kuhusu kunyoa sehemu ya kichwa na kuacha sehemu nyingine

Swali: Ni ipi hukumu ya kunyoa sehemu ya kichwa na kuacha sehemu nyingine?

Jibu: Wanazuoni wanaona kuwa inachukiza. Hata hivyo msingi wa makatazo ni uharamu. Huu ndio msingi. an-Nawawiy ametaja kuwa wanazuoni wanaona kuwa inachukiza. Lakini mtu anaweza kuhoja ni kipi kilichogeuza?

Jibu: Je, kuna dalili inayosema kwamba kisogo ni katika matendo ya waabudia moto?

Jibu: Allaah ndiye mjuzi zaidi. Inatosha kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza jambo hilo. Inatosha.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24107/حكم-القزع-حلق-بعض-الراس-وترك-بعضه
  • Imechapishwa: 31/08/2024