Ndugu yangu Shaykh ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Aamir al-Ahmariy ambaye ninampenda kwa ajili ya Allaah amenitumia kitabu chake ambapo amewaraddi Haddaadiyyah na Shaykh wao Mahmuud al-Haddaad ambaye ameruka mipaka hukumu dhidi ya watu wa Bid´ah wote na kusema ya kwamba haijuzu kuwaombea msamaha na rehema au kusoma vitabu vyao. Kwa njia hiyo anajifananisha na Khawaarij pindi wanapomfanyia Takfiyr mtenda madhambi. Kwa sababu lau tutasema kuwa ni haramu kumuombea rehema na msamaha mtu wa Bid´ah ambaye sio kafiri, tunatangamana naye kama kafiri. Shaykh ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Aamir al-Ahmariy ameandika kitabu “an-Nuquulaat as-Salafiyyah fiyr-Radd ´alaal-Haddaadiyyah” na kunitumia. Nimekisoma chote. Nimekipenda wakati amepata utangulizi wa kina na ameraddi nukta kumi na tatu. Radd yake ni nzuri kwa kuwa ameraddi kila nukta kwa mapokezi kutoka kwa Salaf. Ninawanasihi wanafunzi kusoma kitabu chake kwa sababu kina manufaa.
- Muhusika: ´Allaamah Ahmad bin Yahyaa an-Najmiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Utangulizi wa “an-Nuquulaat as-Salafiyyah fiyr-Radd ´alaa at-Twaaifah al-Haddaadiyyah”, uk. 5-6
- Imechapishwa: 18/05/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)