Swali: Ni ipi hukumu ya kufanya Khuruuj na Jamaa´at-ut-Tabliygh?

Jibu: Usifanye Khuruuj na Jamaa´at-ut-Tabliygh. Kama unataka usalama shikamana na uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kupita juu yake.

Jambo lenye kustaajabisha, ni kwamba Da´wah inakuja hapa, na sio kutoka hapa, wakati ujumbe ulikuja katika nchi hii.

Jamaa´at-ut-Tabliygh hawazungumzii kuhusu Qur-aan na Sunnah. wanazungumzia kuhusu Fiqh. Hawazungumzii kuhusu Tawhiyd. Wanasema kuwa kuna maoni tofauti juu ya masuala hayo na hawataki kuyaingia.

Wana kanuni sita ambazo muasisi wao, Muhammd Ilyaas, ameziweka. Amezikwa kwenye Msikiti wake.[1] Wanatekeleza kanuni hizi sita. Ukiingia katika tafsiri za Qur-aan, wanasema kuwa wao hawaingii katika hayo. Kadhalika wanasema juu ya tafsiri za Hadiyth. Kadhalika wanasema juu ya ufafanuzi wa ´Aqiydah. Kadhalika wanasema juu ya ufafanuzi wa Fiqh. Kwa hakika mimi sijui wanawafunza nini watu. Mtu aulize kuhusu uongofu wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na aufuate.

Nimeona jinsi watu hawa wanafanya mazoezi ya kutoka siku moja, halafu siku tatu, halafu wiki moja, halafu mwezi mmoja na halafu miezi mitatu. Hatimae anatoka na kwenda nao. Mwisho wake anaondokewa na mali zake, watoto wake na mke wake. Hili limewapitikia watu wengi.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan al-Ghudayyaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluum ash-Shar´iyyah li Twaalib-il-´Ilm
  • Imechapishwa: 23/04/2015