Ameswali nchikavu bila ya kufanya bidii yoyote kukitafuta Qiblah

Swali: Vipi ikiwa mtu ataswali nchikavu na asijitahidi kukitafuta Qiblah, alichofanya ni kuanza kuswali wakati tu alipofika.

Jibu: Ikiwa hakufanya juhudi, anapaswa kurudia.

Swali: Lakini alikielekea Qiblah bila ya kufanya juhudi yoyote?

Jibu: Ikiwa alikielekea Qiblah, basi sifa zote njema ni za Allaah.

Swali: Hata kama hakufanya bidii yoyote?

Jibu: Hata kama; muda wa kuwa ameswali akiamini huko ndiko kwenye Qiblah, sifa zote njema ni stahiki ya Allaah. Hilo ndio lengo.

Swali: Hapana, aliswali namna hii tu. Baada ya kuambiwa atafute Qiblah akasema kuwa hapana haja.

Jibu: Maadamu aliswali akiamini huko ndio kwenye Qiblah, sifa zote njema ni za Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27459/حكم-من-صلى-في-البر-ولم-يجتهد-في-القبلة
  • Imechapishwa: 10/04/2025