Ameswali kwa kutumia maji ya tenki yaliyo na mzoga

Swali: Kuna mtu ameswali zaidi ya siku moja kwa wudhuu´ kutoka kwenye tenki. Kisha baada ya hapo akaja kujua kuwa katika tenki hii ya maji kuna mzoga aliyekufa ndani. Ni ipi hukumu ya swalah yake aliyoswali?

Jibu: Ikiwa maji hayakubadilika kwa mzoga huu aliyekufa ndani yake – si ladha yake, harufu yake wala rangi yake – basi ni masafi. Ama ikiwa yalibadilika basi ni najisi. Kujengea juu ya hili mtu huyu atalazimika kurudi swalah yake na aoshe mavazi yake na mwili wake kutokamana na maji haya ambayo ni najisi. Azirudi swalah zake kwa wudhuu´ sahihi.  Lakini ikiwa hayakubadilika hakuna neno juu yake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (44) http://binothaimeen.net/content/1004
  • Imechapishwa: 13/01/2019