Ameswali Dhuhr Rak´ah mbili kisha akakumbushwa

Swali: Aswali Dhuhr Rak´ah mbili kisha akakumbushwa. Je, inafaa kwake kuleta Takbiyrat-ul-Ihraam na du´aa ya kufungulia swalah au aswali tu zile Rak´ah mbili zilizobakia moja kwa moja?

Jibu: Aswali zile Rak´ah mbili zilizobakia moja kwa moja na itatosha. Zitaanzwa na Takbiyr.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23603/هل-يستفتح-من-سها-عن-ركعة-او-اكثر-ثم-تنبه
  • Imechapishwa: 24/02/2024