Swali 633: Vipi ikiwa muislamu ameshindwa kutimiza nadhiri ya kufunga?

Jibu: Swawm hiyo inachukua mkondo kama wa swawm ya faradhi. Kwa maana ya kwamba atalisha chakula. Ikiwa nadhiri yake haikuwa swawm na akashindwa kuitekeleza, basi inadondoka. Ibn ‘Abbaas (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

”Atatoa kafara ya kiapo.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ibn Baaz, uk. 222
  • Imechapishwa: 15/06/2025
  • Mkusanyaji: Shaykh Abiy Muhammad ´Abdullaah bin Maaniy´