Swali: Mtu ameuza mtende wake na akasahau kuitolea zakaah. Je, anunue tende na kuzitoa zakaah au atoe zakaah pesa?

Jibu: Mtu akiuza matunda ya mtende au mazao yake, basi atatoa zakaah ya ile thamani yake. Kwa sababu kufanya hivo ndio karibu zaidi na kufanya uadilifu na ndio jambo linalowanufaisha zaidi mafukara hii leo. Kwa mfano ukiuza mazao kwa 10.000, basi utatoa zakaah ya 5%. Kwa maana nyingine pesa 500.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/85)
  • Imechapishwa: 15/05/2026