Amesahau kutoa Zakaat-ul-Fitwr kabla ya swalah ya ´iyd

Swali: Nilitayarisha Zakaat-ul-Fitwr kabla ya ´iyd ili nimpe nayo fakiri ninayemjua. Lakini nilisahau kuitoa na nikakumbuka kuitoa baada ya swalah ya ´iyd. Ni ipi hukumu?

Jibu: Hapana shaka kuwa ni lazima kuitoa Zakaat-ul-Fitwr kabla ya swalah ya ´iyd. Hivo ndivo alivoamrisha Mtume mtukufu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini hapana ubaya kwako kwa yale uliyoyafanya. Kuitoa baada ya swalah kunasihi, ingawa imepokelewa katika Hadiyth kwamba ni swadaqah miongoni mwa swadaqah. Hata hivyo hilo halizuilii kule kusihi na kwamba imeangukia mahali pake. Tunatumai kuwa ni yenye kukubaliwa na kwamba itakuwa ni zakaah kamili. Kwa sababu hukuichelewesha kwa kukusudia. Umeichelewesha kwa kusahau. Allaah (Ta´ala) amesema:

رَبَّنَا لَا تُؤَاخِذْنَا إِن نَّسِينَا أَوْ أَخْطَأْنَا

“Ee Mola wetu! Usituchukulie pale tutaposahau au tukikosea.”[1]

Imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kuwa amesema: “Allaah (Ta´ala) amesema:

“Nimekwishafanya.”

Kwa hivyo ameitikia du´aa ya waja Wake wema kutowachukulia kwa kusahau na kwa kukosea.

[1] 02:286

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/216)
  • Imechapishwa: 30/04/2022