Amepata kujua kuwa vyombo vya dhahabu na fedha havijuzu

Swali: Ni vipi mtu atafanya kwa mujibu wa Shari´ah kama yuko na vyombo vya jikoni vya dhahabu na fedha kisha akajua kuwa ni haramu?

Jibu: Ni sahali. Aende kwa fundi na amuombe amuondolee dhahabu.

Swali: Anaweza kuwauzia makafiri?

Jibu: Hapana. Asiwauzie na wala asile thamani yake. Ni kama tulivyosema aende kwa fundi amuondolee hiyo dhahabu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (03) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/omdah–14340316.mp3
  • Imechapishwa: 25/08/2020