Ameona kiungo fulani hakikupata maji

Swali: Ikiwa ataona sehemu haikupata maji kwenye kisigino akiwa ndani ya swalah anatakiwa kutoka kwenye swalah na kurudia wudhuu´?

Jibu: Ndio, ikiwa ameona sehemu hiyo, basi wudhuu´ wake ni batili. Kufuatanisha viungo kumevunjika. Kwa hivyo anatakiwa kurudia wudhuu´.

Swali: Vipi ikiwa ataiona baada ya kumaliza swalah yake?

Jibu: Arudie wudhuu´ na pia arudie swalah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31517/ماذا-يفعل-من-راى-لمعة-في-عقبه-لم-يصلها-الماء
  • Imechapishwa: 30/10/2025