Amemtanga mkewe na badala yake anafanya punyeto

Swali: Dada muulizaji kutoka Uingereza anasema. Kuna mwanamke anauliza kuhusu mume wake anafanya punyeto kwa muda wa miaka nne na amemtenga na huyo dada amemvumilia. Mwanaume huyo ni mwenye msimamo na ni Salafiy. Pamoja na kujua ya kwamba yeye [mume] anafikiria ya kwamba mke wake hajui. Unamnasihi nini ee Shaykh?

Jibu: Haijuzu kwa yeyote kufanya punyeto, sawa ikiwa ameoa au ni kijana hajaoa. Kutokana na madhara yanayopatikana kwa kufanya hivyo ya kidini na ya kiafya. Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

فَمَنِ ابْتَغَىٰ وَرَاءَ ذَٰلِكَ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْعَادُونَ إِلَّا عَلَىٰ أَزْوَاجِهِمْ أَوْ مَا مَلَكَتْ أَيْمَانُهُمْ فَإِنَّهُمْ غَيْرُ مَلُومِينَ

“Isipokuwa kwa wake zao au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi hao hawalaumiwi. Basi yeyote yule atakayetaka kinyume ya hayo, basi hao ndio wavukao mipaka.” (70:29-30)

yaani mwenye kutafuta kukidhi shahawa zake kwa asiyekuwa mke wake au yule iliyowamiliki mikono yao ya kuume, basi huyo ni wale warukao mipaka. Anaingia katika hiyo [Aayah] watu wenye kufanya punyeto ambao wanatumia mikono yao. Na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Enyi kongamano la vijana! Yule miongoni mwenu mwenye uwezo wa kuoa na afanye hivyo, kwani hilo linamfanya ainamishe macho yake na inahifadhi utupu wake. Ama kwa yule asiyeweza basi afunge… “

Na wala hakumwelekeza kwenda kufanya punyeto. Maoni yenye nguvu miongoni mwa maoni ya wanachuoni ni kwamba kufanya punyeto ni haramu. Mwenye kutumbukia ndani yake akimbilie kufanya tawbah. Allaah huyabadili mabaya kuwa mema. Atahadhari kuendelea baada ya kumbainishia haki. Na huyu mwanamke ameshamnasihi na ni juu yake [huyo mwanamke] kumfikishia aliyosikia. Na ni wajibu kwake kumcha Allaah (´Azza wa Jall). Allaah kamtajirisha kwa kumpa mke. Ni madai yapi aliyo nayo ya kumpelekea akafanya kunyeto? Hana lolote zaidi ya kufuata matamanio yake na mahitajio ya nafsi inayoamrisha maovu.

Check Also

Mke anachukua pesa kutoka kwa mume kwa ajili ya haja za mustakabali

Swali: Mke anachukua pesa kutoka kwa mume wake na anasema kuwa ni kwa ajili ya …