Amempa zawadi baada ya kumsaidia kazi

Swali: Mtu anafanya kazi katika idara fulani ambaye akamsaidia mtu mwingine kumaliza kazi yake katika idara hiyo. Baada ya kumaliza kazi yule mtu akampa zawadi ya vitabu ambavyo vimeandikwa “Waqf kwa ajili ya Allaah (Ta´ala)”. Ni ipi hukumu ya jambo hili? Je, hii ni rushwa au ni nini?

Jibu: Mfanyakazi anayeshughulikia kumaliza kazi ya ndugu yake hapaswi kuchukua rushwa, kuchukua mali na wala kuchukua zawadi yoyote, kwa sababu mara nyingi jambo hili huwa ni hongo kwa jina la zawadi. Hata kama ni vitabu vilivyowekwa waqf kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), basi haruhusiwi kuchukua chochote kabisa. Kwa kuwa mara nyingi hilo huwa ni njia ya rushwa ili amsaidie kwa kumpa upendeleo juu ya wengine, kuchelewesha kazi za watu wengine, kumpa haki isiyokuwa yake au kumfanyia mambo kinyume na haki. Hivyo mfanyakazi hapaswi kupokea kitu chochote kabisa katika hali kama hii.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3164/حكم-الهدية-مقابل-خدمة-معاملة-في-مكتب-ادارة
  • Imechapishwa: 26/07/2026