Swali: Mtu amepata mali kwa wizi na rushwa, lakini anafanya matendo mema kama swadaqah, Hajj, ´Umrah, zakaah na matendo mengi ya kheri. Je, matendo hayo yanafuta madhambi aliyoyapata kutokana na uovu wake?
Jibu: Hapana. Bado anabaki na haki za watu aliowadhulumu kwa rushwa na wizi. Haitoshi kufanya matendo hayo mema tu, ni lazima arudishe haki kwa wenyewe. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh akiwauliza Maswahabah zake:
“Mnamhesabu nani kuwa ni mtu aliyefilisika miongoni mwenu?” Wakasema: ”Ni yule asiye na dirhamu wala mali.” Akasema: “Lakini aliyefilisika katika ummah wangu ni yule anayekuja siku ya Qiyaamah hali ya kuwa amemtukana huyu, amempiga huyu, amechukua mali ya huyu, amemwaga damu ya huyu na amemsingizia machafu huyu. Basi huyu atapewa katika mema yake na huyu atapewa katika mema yake. Yakimalizika mema yake kabla hajamaliza haki alizonazo, basi atachukuliwa katika maovu yao na kubebeshwa yeye, kisha atatupwa Motoni.”
Hivyo ni lazima arudishe haki za watu.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3159/حكم-من-يعمل-الصالحات-لكن-كسبه-حرام
- Imechapishwa: 26/07/2026
Swali: Mtu amepata mali kwa wizi na rushwa, lakini anafanya matendo mema kama swadaqah, Hajj, ´Umrah, zakaah na matendo mengi ya kheri. Je, matendo hayo yanafuta madhambi aliyoyapata kutokana na uovu wake?
Jibu: Hapana. Bado anabaki na haki za watu aliowadhulumu kwa rushwa na wizi. Haitoshi kufanya matendo hayo mema tu, ni lazima arudishe haki kwa wenyewe. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth Swahiyh akiwauliza Maswahabah zake:
“Mnamhesabu nani kuwa ni mtu aliyefilisika miongoni mwenu?” Wakasema: ”Ni yule asiye na dirhamu wala mali.” Akasema: “Lakini aliyefilisika katika ummah wangu ni yule anayekuja siku ya Qiyaamah hali ya kuwa amemtukana huyu, amempiga huyu, amechukua mali ya huyu, amemwaga damu ya huyu na amemsingizia machafu huyu. Basi huyu atapewa katika mema yake na huyu atapewa katika mema yake. Yakimalizika mema yake kabla hajamaliza haki alizonazo, basi atachukuliwa katika maovu yao na kubebeshwa yeye, kisha atatupwa Motoni.”
Hivyo ni lazima arudishe haki za watu.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3159/حكم-من-يعمل-الصالحات-لكن-كسبه-حرام
Imechapishwa: 26/07/2026
https://firqatunnajia.com/aliyefisika-katika-ummah-wa-muhammad/