Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
3 – Uhakika wa linavyoishilia jambo, hata kama unaafikiana na udhahiri wake. Uhakika wa yale aliyoeleza Allaah kuhusu chakula cha Peponi, kinywaji, mavazi, ndoa, kusimama kwa Qiyaamah na mengineyo, kunakusudiwa uhakika wake, na si ile maana ambayo mtu anaifikiria akilini mwake au akaizungumza wazi kwa mdomo. Hii ndio tafsiri ya neno (التأويل) kwa mujibu wa lugha ya Qur-aan. Allaah (Ta´ala) amesema ya kwamba Yuusuf (´alayhis-Salaam) amesema:
يَا أَبَتِ هَـٰذَا تَأْوِيلُ رُؤْيَايَ مِن قَبْلُ قَدْ جَعَلَهَا رَبِّي حَقًّا
“Ee baba yangu! Hii ni tafsiri ya njozi yangu hapo kabla, Mola wangu ameifanya kuwa ya kweli.”[1]
هَلْ يَنظُرُونَ إِلاَّ تَأْوِيلَهُ
“Je, wanangojea nini isipokuwa matokeo yake?”[2]
ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً
“Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”[3]
Hii ndio (التأويل) ambayo hakuna anayeijua isipokuwa Allaah. Allaah pekee ndiye anayejua uhakika wa sifa Zake, nayo ni ile namna isiyotambulika. Salaf, akiwemo Maalik, amesema juu yake:
“Kulingana juu kunajulikana. Namna haijulikani.”[4]
MAELEZO
Yale yaliyotokea katika kusujudu wazazi wake na ndugu zake kumi na mmoja ndiyo tafsiri ya ndoto yake aliyoiona alipokuwa mdogo. Hakujua tafsiri yake isipokuwa ilipotokea. Vivyo hivyo yaliyoko Aakhirah hayatajulikana isipokuwa yatakapoonekana siku ya Qiyaamah. Hii ndiyo tafsiri, kwa maana kile jambo linaishia kwake katika hakika yake iliyofichika kwetu. Allaah (Ta´ala) amesema:
هَلْ يَنظُرُونَ إِلاَّ تَأْوِيلَهُ
“Je, wanangojea nini isipokuwa matokeo yake?”
Kwa maana makafiri hawangoji jengine isipokuwa uhalisia wake. Kwa msemo mwingine kutokea kwa yale yaliyokuja ndani ya Qur-aan ambayo Allaah ameyaeleza, kama siku ya Qiyaamah na yaliyomo humo katika Pepo na Moto. Wakati huo ndipo watakapogundua kwamba walikosea duniani:
هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّا تَأْوِيلَهُ ۚ يَوْمَ يَأْتِي تَأْوِيلُهُ يَقُولُ الَّذِينَ نَسُوهُ مِن قَبْلُ قَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ فَهَل لَّنَا مِن شُفَعَاءَ فَيَشْفَعُوا لَنَا أَوْ نُرَدُّ فَنَعْمَلَ غَيْرَ الَّذِي كُنَّا نَعْمَلُ
“Je, wanangojea nini isipokuwa matokeo yake? Siku yatakapofika matokeo yake watasema wale walioisahau hapo kabla “hakika Mitume wa Mola wetu walikuja kwa haki. Je, tuna waombezi wowote watuombee au turudishwe [ulimwenguni] ili tufanye kinyume na yale tuliyokuwa tukifanya?”[5]
Wakati huo watatambua ukweli wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) baada ya kuona kwa macho yao hakika ya yale waliyowaeleza. Walikuwa ulimwenguni wakiwakadhibisha, lakini watakapoyaona siku ya Qiyaamah watasema:
قَدْ جَاءَتْ رُسُلُ رَبِّنَا بِالْحَقِّ
“Hakika Mitume wa Mola wetu walikuja kwa haki.”
Haya ndiyo waliotuambia Mitume wetu, lakini majuto ni mjukuu.
Vilevile Allaah (Ta´ala) amesema:
ذَلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلاً
“Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”
Kwa maana matokeo bora zaidi. Kurejesha mzozo katika Qur-aan na Sunnah ndiyo mwisho bora kabisa. Hii inafahamisha kuwa tafsiri inaweza kuwa na maana ya mwisho na matokeo. Tafsiri hii (التأويل) ndio ambayo hakuna anayeijua isipokuwa Allaah tu, kwa sababu hayo ni katika elimu ya ghaibu. Hakika za majina na sifa za Allaah, hakika za yaliyomo Peponi na Motoni na mambo yatakayotokea siku ya Qiyaamah yote yamefichika kwetu.
Kutokana na maana hii tafsiri ya sifa ni hakika yake na namna yake ilivyo. Elimu hii hakuna aijuaye isipokuwa Allaah tu. Hata hivyo sisi tunajua tafsiri yake. Ndiyo maana Salaf walikuwa wakisema kuwa maana yake inajulikana na namna yake haijulikani. Hii ni kanuni kubwa sana kwamba maana ya Sifa tunaijua, lakini namna yake haijulikani. Hivo ndivo alivyosema Imaam Maalik (Rahimahu Allaah), Rabiy´ah, Umm Salamah na wengineo katika Salaf.
[1] 12:100
[2] 7:53
[3] 4:59
[4] al-Bayhaqiy katika ”Kitaab-ul-Asmaa’ was-Swifaat” (867) na (868), ad-Daarimiy katika ”ar-Radd ´alaa al-Jahmiyyah” (104), al-Laalikaa’iy (664) na wengineo.
[5] 07:53
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 262-265
- Imechapishwa: 27/07/2026

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 262-265
Imechapishwa: 27/07/2026
https://firqatunnajia.com/161-tafsiri-hii-hakuna-anayeijua-isipokuwa-allaah/