Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kulingana juu inajulikana maana yake na kunafasiriwa na kufanyiwa tarjama kwa lugha nyingine. Aidha ni miongoni mwa tafsiri zinazotambulika na wale wanzuoni waliobobea katika elimu. Lakini namna ya kulingana haijulikani. Allaah pekee ndiye anajua (التأويل) yake.
MAELEZO
Kulingana juu kunatambulika. Kulingana juu ya ´Arshi maana yake ni kuwa ameinuka na kupaa juu yake. Mmea uliposimama juu ya mashina yake maana yake ni kuinuka kwake juu ya mashina yake. Maana yake katika lugha ni ujuu na uinukaji. Hata hivyo hatujui namna ya kulingana kwa Allaah juu ya ´Arshi Yake. Sisi tunasema kuwa Allaah amelingana na kupaa juu ya ´Arshi, lakini namna yake haijulikani isipokuwa kwa Allaah. Neno hilo linaweza kutafsiriwa kutoka lugha ya kiarabu kwenda lugha nyingine, kwa sababu maana yake inajulikana. Lau isingejulikana, isingewezekana kuitafsiri. Vivyo hivyo kuhusiana na Hadiyth isemayo:
Abu Hurayrah ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika Allaah (Ta´ala) hushuka katika mbingu ya chini wakati kunapobaki nusu ya usiku, au theluthi ya mwisho ya usiku, na akasema mpaka kupambazuke alfajiri, au mpaka pale msomaji anapoondoka katika swalah ya asubuhi: ”Nani anayeniomba Nimpe? Ni nani anayeniuliza Nimpe? Ni nani anayenitaka msamaha Nimsamehe? Ni nani anayetaka nimsamehe Nimghufurie?”
Kwa maana kushuka kunajulikana na huwa kutoka juu kwenda chini. Ama namna Allaah anavyoshuka, hilo halijulikani isipokuwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 266
- Imechapishwa: 27/07/2026
Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:
Kulingana juu inajulikana maana yake na kunafasiriwa na kufanyiwa tarjama kwa lugha nyingine. Aidha ni miongoni mwa tafsiri zinazotambulika na wale wanzuoni waliobobea katika elimu. Lakini namna ya kulingana haijulikani. Allaah pekee ndiye anajua (التأويل) yake.
MAELEZO
Kulingana juu kunatambulika. Kulingana juu ya ´Arshi maana yake ni kuwa ameinuka na kupaa juu yake. Mmea uliposimama juu ya mashina yake maana yake ni kuinuka kwake juu ya mashina yake. Maana yake katika lugha ni ujuu na uinukaji. Hata hivyo hatujui namna ya kulingana kwa Allaah juu ya ´Arshi Yake. Sisi tunasema kuwa Allaah amelingana na kupaa juu ya ´Arshi, lakini namna yake haijulikani isipokuwa kwa Allaah. Neno hilo linaweza kutafsiriwa kutoka lugha ya kiarabu kwenda lugha nyingine, kwa sababu maana yake inajulikana. Lau isingejulikana, isingewezekana kuitafsiri. Vivyo hivyo kuhusiana na Hadiyth isemayo:
Abu Hurayrah ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Hakika Allaah (Ta´ala) hushuka katika mbingu ya chini wakati kunapobaki nusu ya usiku, au theluthi ya mwisho ya usiku, na akasema mpaka kupambazuke alfajiri, au mpaka pale msomaji anapoondoka katika swalah ya asubuhi: ”Nani anayeniomba Nimpe? Ni nani anayeniuliza Nimpe? Ni nani anayenitaka msamaha Nimsamehe? Ni nani anayetaka nimsamehe Nimghufurie?”
Kwa maana kushuka kunajulikana na huwa kutoka juu kwenda chini. Ama namna Allaah anavyoshuka, hilo halijulikani isipokuwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaa al-Hamawiyyah, uk. 266
Imechapishwa: 27/07/2026
https://firqatunnajia.com/162-maana-inatambulika-namna-haitambuliki/