Amempa wasia wa nyumba mke lakini watoto hawako radhi kwa hilo

Swali: Mwanamke alimuuliza mume wake mzee sana kwa mzaha kwamba ampe nyumba miongoni mwa nyumba zake baada ya kufa kwake, naye akakubali ombi hilo na watoto wa mtu huyu hawaridhii zawadi hiyo. Ni kana kwamba wanapinga jambo hilo. Watoto wa ndugu wa mtu huyu waliandika wasia huo na wakamuuliza tena ambapo akasema kuwa yeye ameridhia hilo. Ni ipi hukumu ya hilo? Je, nyumba itakuwa ya mke au vipi?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Hakika Allaah amempa kila mwenye haki haki yake. Hivyo basi hakuna wasia kwa mrithi.”

Kwa hiyo hana wasia. Ikiwa amemuusia mke wake nyumba au fedha, basi wasia ni batili, isipokuwa warithi wautekeleze. Ikiwa warithi waliokomaa na wenye akili wataridhia na kuutekeleza, basi hakuna ubaya. Vinginevyo hana haki isipokuwa yale aliyompa Allaah. Ana haki ya theluthi ya nane pamoja na watoto ikiwa ni mmoja. Ana haki ya nusu ya theluthi ya nane pamoja na watoto ikiwa ni wawili. Ana haki ya theluthi ya theluthi ya nane ikiwa ni watatu. Ana haki ya robo ya theluthi ya nane ikiwa ni wa nne pamoja na watoto. Ikiwa hana watoto, basi anapata robo. Ikiwa ni wawili basi robo inagawanywa kati yao. Ikiwa ni watatu basi kwa theluthi baina yao na vivyo hivyo wanne. Ninachotaka kusema ni kwamba hana wasia isipokuwa warithi wakiruhusu na wakampa. Katika hali hiyo hakuna ubaya, ikiwa ni watu waliobaleghe na wenye akili timamu.

Swali: Hata kama wasia umetoka katika theluthi?

Jibu: Katika theluthi au nje ya theluthi, hapana neno ikiwa amemuusia na wao wakaridhia.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3384/الوصية-للزوجة-وعدم-موافقة-الاولاد-على-ذلك
  • Imechapishwa: 15/09/2026