131 – Nuswayr bin al-Faraj amenikhabarisha: Shu´ayb bin Harb ametuhadithia, kutoka kwa ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Abiy Salamah: Muhammad bin al-Munkadir ametuhadithia, kutoka kwa Jaabir bin ´Abdillaah, ambaye amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Nilioteshwa jinsi nilivyoingia Peponi ambapo nikasikia hatua mbele yangu. Nikasema: “Ni nani huyo, ee Jibriyl?” Akasema: ”Ni Bilaal.” Nikaona kasri ambalo uani alisimama mwanamke kijana. Nikasema: “Ni ya nani hii, ee Jibriyl?” Akasema: “Ni ya ´Umar bin al-Khattwaab.”[1]

132 – Muhammad bin ´Abdillaah bin al-Mubaarak ametukhabarisha: Abu Usaamah ametukhabarisha: Abu Hayyaan amenikhabarisha, kutoka kwa Abu Zur´ah, kutoka kwa Abu Hurayrah, aliyesema:

“Wakati wa Faje, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) alimwambia Bilaal: “Nambie kitendo ambacho unakitarajia zaidi katika Uislamu. Kwani hakika juzi usiku nilisikia hatua zako mbele yangu Peponi.” Akasema: “Hakuna kitendo chochote nilichofanya katika Uislamu ninachokitarajia zaidi kwamba kamwe sijatia twahara kamilifu, bila ya kujali muda wa mchana au wa usiku, isipokuwa baada ya hapo nimemuomba Mola wangu kile alichoniandikia kuswali.”[2]

133 – Ishaaq bin Ibraahiym ametukhabarisha: ´Ubaydullaah bin Muusa ametukhabarisha: Israaiyl ametukhabarisha, kutoka kwa al-Miqdaam bin Shurayh, kutoka kwa baba yake, kutoka kwa Sa´d bin Abiy Waqqaas, ambaye amesema:

“Tulikuwa watu sita pamoja na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam). Wakasema: ”Wafukuze watu hawa kutoka kwako. Wako na haya na yale.” Alikuwa mimi, Ibn Mas´uud, bwana mwingine anayetokea Hudhayl, Bilaal na mabwana wengine wawili ambao nimesahau majina yao. Kukaingia kitu katika mawazo alichotaka Allaah, ambapo Allaah akateremsha:

وَلَا تَطْرُدِ الَّذِينَ يَدْعُونَ رَبَّهُم بِالْغَدَاةِ وَالْعَشِيِّ يُرِيدُونَ وَجْهَهُ ۖ مَا عَلَيْكَ مِنْ حِسَابِهِم مِّن شَيْءٍ وَمَا مِنْ حِسَابِكَ عَلَيْهِم مِّن شَيْءٍ فَتَطْرُدَهُمْ فَتَكُونَ مِنَ الظَّالِمِينَ

“Na wala usiwafukuze wale wanaomwomba Mola wao asubuhi na jioni wanataka uso Wake. Si juu yako hesabu yao chochote na wala hesabu yako si juu yao chochote, hata uwafukuze, [kwani ukiwafukuza] utakuja kuwa miongoni mwa madhalimu.”[3]

[1] al-Bukhaariy (3242) na Muslim (2395).

[2] al-Bukhaariy (1149) na Muslim (2458).

[3] 6:52 Muslim (2413).

  • Muhusika: Imaam Ahmad bin Shu´ayb an-Nasaa’iy (afk. 303)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwaa-il-us-Swahaabah, uk. 94-95
  • Imechapishwa: 15/09/2026