Amekumbuka kuwa hakuswali Maghrib pindi yuko anaswali ´Ishaa

Swali: Nilichelewesha Maghrib na ´Ishaa kwa sababu nilikuwa msafiri. Nikaswali ´Ishaa na mkusanyiko wa msikitini na nikasahau kuswali Maghrib, na nikakumbuka hilo katika Tashahhud ya mwisho katika swalah ya ´Ishaa. Je, nifanye ´Ishaa kisha Maghrib pamoja na kujua kuwa Rakaa´ moja ilinipita au niswali Maghrib halafu ndio niswali ´Ishaa?

Jibu: Hapana, usiswali ´Ishaa kabla ya Maghrib. Hata hivyo ni sawa endapo utasahau kuswali Maghrib na ukakumbuka hilo baada ya kuwa umeshaswali ´Ishaa. Katika hali hii utaswali Maghrib baada ya ´Ishaa.

Ama ukikumbuka wakati uko unaswali ´Ishaa basi unachotakiwa ni wewe kuifanya kuwa swalah ya Sunnah kisha baada ya hapo uswali Maghrib halafu ´Ishaa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-qrran-19-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020