Amekuja Jeddah kimatembezi kisha akahirimia hapo kwa ajili ya Hajj

Swali: Mtu alisafiri siku za Hajj kutoka Riyaadh kwenda Madiynah, hali ya kuwa si mwenye kuhirimia, kisha akasafiri kutoka Madiynah kwenda Jeddah na akakaa humo siku kumi na tano akiwa amesafiri kwa ndege kutoka makazi yake Riyaadh. Hakuwa na nia ya Hajj bali ya matembezi tu. Ilipofika siku za Hajj akataka kuhiji ambapo akahiji na kukamilisha Hajj yake. Je, analazimika kuchinja mnyama wa Hadiy kwa kuwa yeye ni mkazi wa Riyaadh na alihirimia kutoka kituo cha Jeddah? Je, Jeddah ni katika kituo?

Jibu: Hapana, halazimiki chochote, muda wa kuwa alikuja Jeddah bila kukusudia Hajj wala ´Umrah, bali kwa ajili ya matembezi tu, kisha Hajj ikamkuta akiwa huko na akahirimia Hajj tu bila kufanya ´Umrah, basi hana fidia yoyote. Ama ikiwa alihirimia ´Umrah kutoka Jeddah, akakamilisha ´Umrah, kisha akahirimia Hajj au akahirimia zote mbili pamoja kutoka Jeddah, basi atawajibika kuchinja Hadiy kwa sababu anakuwa ametekeleza Hajj ya Tamattu´. Lakini ikiwa alihirimia Hajj peke yake kutoka Jeddah ambayo ikakutana na Hajj akiwa huko ambapo akaingia Ihraam kutoka huko, basi hakuna ubaya juu yake na atahesabiwa kuwa ni mwenye kufanya Hajj ya Ifraad.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3293/حكم-من-جاء-الى-جدة-للزيارة-ثم-احرم-منها-للحج
  • Imechapishwa: 08/08/2026