Swali: Mmoja wa maimamu wa misikiti amenituma niwaulize kuhusu maandishi yanayoning’inizwa misikitini, kama Aayah na Hadiyth. Je, hilo linajuzu?

Jibu: Wanazuoni wengi wanaona ni jambo linalochukiza kufanya hivyo misikitini, kwa sababu huenda likawashawishi waswaliji khaswa ikiwa yapo upande wa Qiblah ya wanaoswali. Hivyo haifai kuning’iniza maandishi upande wa Qiblah cha wanaoswali, kwa sababu yanaweza kuwachanganya watu na kumshughulisha anayeswali.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3297/حكم-تعليق-الايات-والاحاديث-في-المساجد
  • Imechapishwa: 08/08/2026