Amekaa na mke mwaka mzima baada ya kumtaliki

Swali: Kuna mtu amemtaliki mke wake na yuko ananyonyesha. Wakakaa pamoja baada ya kuachana mwaka mzima. Je, talaka hii ni sahihi au si sahihi?

Jibu: Baada ya kumtaliki anatakiwa kumwepuka. Amtaliki kabla ya kumwingilia. Akimtaliki baada ya kumwingilia, hiyo ni dhambi na haijuzu. Hivo ndivo alivosema Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisema:

”Kisha  mbakize mpaka atwahirike.”

Anatakiwa kumtaliki kabla hajamwingilia.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (18)
  • Imechapishwa: 02/01/2021