Amefika Muzdalifah baada ya jua kuzama

Swali: Nilifika Muzdalifah baada ya jua kuzama kwa sababu ya msongamano mkubwa wa watu. Je, ni lazima nitoe fidia?

Jibu: Ikiwa unasafiri kwenda Muzdalifah na ukazuiwa na msongamano mkubwa wa watu, hakuna kinachokulazimu. Kwa sababu ni mwenye kupewa udhuru.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (23) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Umdah-13-2-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 27/06/2020