Swali: Mimi ni mwanamke nimeolewa na nina watoto wa kiume wawili na mume wangu haswali kabisa mpaka swalah ya ijumaa. Je, inafaa kwangu kuomba talaka pamoja na kuzingatia kwamba niko nyumbani kwa familia yangu kutokana na sababu hii?

Jibu: Ikiwa mume wako haswali basi ndoa ni batili. Haisihi kwako kubaki kwake. Ni lazima kwa mwanamke kujitenga naye na usimkurubie. Vivyo hivyo ikiwa mwanamke yeye ndiye haswali basi ni kwa mume kutomkurubia. Kwa sababu mwanamke huyo atakuwa ni kafiri. Mwenye kuacha swalah anakufuru kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule atakayeiacha amekufuru.”

Kwa hivyo mwanamme akiacha swalah kwa makusudi au mwanamke akaacha swalah kwa makusudi anakufuru. Mwanamme hatomkurubia akiwa yeye mwanamke haswali na kadhalika mwanamke hatomkurubia ikiwa yeye mwanamme haswali. Bali mwanamke atajiepusha naye na kwenda kwa familia yake. Anatakiwa kutubia. Akitubia na akajirudi basi inafaa kwa mume kurejea kwa mwanamke huyo. Vivyo hivyo ikiwa mwanamke ndiye haswali basi anatakiwa kujiepusha naye na amnasihi na kumtia adabu. Akitubia, ni vyema, na vinginevyo mwanamke huyo hatohalalika kwa mwanamme huyo. Hili ndilo la wajibu. Swalah ndio nguzo ya Uislamu.

Yule anayekanusha uwajibu wake basi anakufuru kwa maafikiano ya waislamu. Yule atakayeiacha kwa kuzembea basi anakufuru kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule atakayeiacha amekufuru.”

Amesema tena (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Baina ya mtu na shirki na ukafiri na shirki ni kuacha swalah.”

Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.

Vilevile amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuhusu viongozi alipoulizwa juu yao: “Je, si tuwapige vita?” Akasema: “Hapana, mpaka muone ukafiri wa wazi ambao mna dalili juu yake kutoka kwa Allaah.”

Imekuja katika upokezi mwingine:

“Hapana, muda wa kuwa wanasimamisha swalah.”

Hiyo ikajulisha kwamba kutosimamisha swalah ni miongoni mwa ukafiri wa wazi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/4289/ما-حكم-من-كان-زوجها-لا-يصلي
  • Imechapishwa: 06/06/2022