Swali: Je, inafaa kwake kuapa kwamba hatozungumza siku nzima?

Jibu: Haitakiwi kwake kuapa kwamba hatozungumza. Imechukizwa ikiwa amekusudia mazungumzo ya kawaida. Hata hivyo ni haramu na maovu ikiwa amekusudia mazungumzo kama vile kuitikia salamu, Tasbiyh na kisomo cha Qur-aan ambacho ni cha wajibu. Katika hali hiyo atalazimika kukivunja. Lakini kama amekusudia mazungumzo ya kawaida, ambayo sio ya lazima, inachukiza. Ni kama ambavo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwakemea wana wa israaiyl wakati walipoweka nadhiri ya kutozungumza na kusimama kwenye jua.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24422/حكم-من-حلف-الا-يتكلم-يوما-كاملا
  • Imechapishwa: 09/10/2024