Swali: Ambaye amepitwa na swalah ya Fajr pasi na khiyari yake na ni katika watu wenye kuhifadhi Swalah ya Jamaa´ah na hakuamka isipokuwa wakati kunapokimiwa kwa ajili ya swalah ya ijumaa, kisha akaswali ijumaa kwa nia ya Fajr na baada ya hapo akalipa Dhuhr Rak´ah nne. Je, kitendo chake hichi ni sahihi?

Jibu: Hapana, sio sahihi. Alitakiwa kuswali Fajr kwanza Rak´ah mbili kisha ndio akaswali ijumaa. Angeanza kuswali Fajr kisha ndio akaswali ijumaa ijapo ijumaa atawahi Rak´ah ile ya mwisho tu. Anatakiwa kuswali Fajr kwanza Rak´ah mbili kisha aingie pamoja na imamu kwa zile Rak´ah zitazokuwa zimebaki za ijumaa. Ikiwa amewahi Rak´ah moja kikamilifu, aitimize kwa sura ya ijumaa. Ikiwa hakuiwahi [Rak´ah moja] kikamilifu, aitimize kwa sura ya Dhuhr.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (06) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_06.mp3
  • Imechapishwa: 31/05/2015