Swali: Afanye nini ambaye amepitwa na Rak´ah ya swalah ya ijumaa? Je, akamilishe Rak´ah nyingine moja au aiswali Dhuhr?

Jibu: Kama wamekwishaswali Rak´ah moja udhahiri ni kwamba atakamilisha Rak´ah nyingine moja iliyobaki na hivyo ijumaa itakuwa imekamilika. Kama wamekwishaswali Rak´ah zote mbili basi ataiswali Dhuhr ikiwa umekwishaingia wakati wa Dhuhr. Kila mmoja ataswali peke yake. Wakimtanguliza mtu mmoja akawaswalisha basi nataraji kuwa hakuna neno kufanya hivo. Wakimtanguliza mmoja basi watakamilisha swalah Rak´ah nne ikiwa wamewahi kilichopungua chini ya Rak´ah moja. Lakini wakiwahi Rak´ah moja, kama ambaye amekuja amechelewa na akapitwa na Rak´ah moja ya swalah ya ijumaa,  basi wataongeza Rak´ah moja na hivyo swalah ya ijumaa itakuwa imekamilika.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 21/05/2021