Swali: Ni yepi makusudio ya maneno ya Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) aliposema:
“Ni Bid´ah kuuliza juu yake”?
Jibu: Salaf hawakuuliza namna zilivyo sifa za Allaah. Kwa sababu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) pekee ndiye anayejua namna yake. Maswahabah walikaa kimya, wakaitikia, wakaamini na wakasadikisha. Hawakuuliza kuhusu namna ya sifa za Allaah. Namna ni jambo maalum kwa Allaah; hakuna anayejua namna ya sifa Zake isipokuwa Yeye pekee (Subhaanahu wa Ta´ala).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat ´alaal-Fatwaa al-Hamawiyyah al-Kubraa, uk. 59
- Imechapishwa: 06/02/2023