Swali: Je, Allaah anaweza kuonekana ulimwenguni?

Jibu: Hapana, ataonekana Aakhirah peke yake. Waumini watamuona Aakhirah. Amesema kuhusu ulimwenguni:

لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي

“Hutoniona! Lakini tazama jabali. Likitulia mahali pake, basi utaniona.”[1]

Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Tambueni kuwa hakuna yeyote katika nyinyi atakayemuona Mola wake mpaka atapofariki.”

Hata Mtume na Muusa (Swalla Allaahu ´alayhimaa wa sallam) alipotaka kumuona Allaah alimwambia:

لَن تَرَانِي وَلَـٰكِنِ انظُرْ إِلَى الْجَبَلِ فَإِنِ اسْتَقَرَّ مَكَانَهُ فَسَوْفَ تَرَانِي

“Hutoniona! Lakini tazama jabali. Likitulia mahali pake, basi utaniona.”

Lakini Aakhirah waumini watamuona katika uwanja wa mkusanyiko na Peponi.

Swali: Vipi kuhusu maneno ya Ibn ´Abbaas kwamba alimuona kwa moyo wake?

Jibu: Huu ni uonaji wa usingizini. Alimtambua zaidi kwa moyo wake.

[1] 7:143

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22344/هل-يمكن-روية-الله-عز-وجل-في-الدنيا
  • Imechapishwa: 17/02/2023