Allaah atawasamehe baadhi ya watenda madhambi makubwa

Swali: Je, mtu anaweza kusema kwamba katika uadilifu ni wa Allaah ni lazima awaadhibu watenda maasi makubwa kwa njia ya kukata kama alivyokhabarisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Kumepokelewa lukuki ya maelezo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba wataingia Motoni kikosi cha watenda madhambi makubwa na wako wengine ambao watasamehewa. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakika Allaah hasamehi kushirikishwa lakini anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa amtakae.”[1]

Miongoni mwao wako ambao watasamehewa na wengine watafikwa na hali za kutisha na matatizo katika kisimamo cha siku ya Qiyaamah. Miongoni mwao wako ambao wataadhibiwa ndani ya kaburi na hivyo wasiadhibiwe kwa Moto kutokana na hiyo adhabu ya ndani ya kaburi au kutokana na hali za kutisha na matatizo yaliyowafika. Miongoni mwao wako ambao wataingia Motoni. Kumepokelewa maelezo mengi juu ya haya. Lakini hata hivyo watatoka humo kwa uombezi wa waombezi na huruma wa mwingi wa huruma. Hakuna atakayebaki ndani yake isipokuwa makafiri peke yake.

[1] 04:48

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (15)
  • Imechapishwa: 03/12/2020