Swali: Maneno ya Allaah (Subhaanah):

إِلَىٰ رَبِّهَا نَاظِرَةٌ

“Zikimtazama Mola wake.” (75:23)

Je, kuna dalili ya kuthibitisha kuwa Allaah (Subhaanah) Yuko upande wa juu?

Jibu: Ndio, watamuona Mola Wao kwa upande wa juu. Hawatomuona mbele yao. Watamuona kwa upande wa juu. Atajionyesha kwao na wao watamuona. Ni kama mfano wa mwezi na jua, wanaviona kwa juu. Hawavioni kwa kuangalia upande wa ardhi. Wanaviona kwa upande wa juu mbinguni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (49) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1431-6-3.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020