Allaah anazungumza kwa sauti inayosikika

Kuhusu sauti ya Allaah, imepokelewa kupitia kwa ´Abdullaah bin Unays kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:

“Ataita (Subhaanah) kwa sauti itayosikika na wale walioko mbali na wale walioko karibu: “Mimi ndiye Mfalme! Mimi ndiye Mwenye kuhukumu!””[1]

Ameipokea Ahmad na maimamu wengine. al-Bukhaariy ameitumia kama hoja yenye kutilia nguvu.

Ibn Mas´uud ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah anapozungumza kwa Wahy, wakazi wa mbinguni husikia sauti Yake kama vile mnyororo juu ya mlima na hushuka chini wakasujudu.”[2]

Maneno ya mwenye kusema kwamba herufi na sauti haiwi isipokuwa kupitia njia zake ni batili. Allaah (Ta´ala) amesema:

يَوْمَ نَقُولُ لِجَهَنَّمَ هَلِ امْتَلَأْتِ وَتَقُولُ هَلْ مِن مَّزِيدٍ

“Siku Tutakapoiambia Jahannam: “Je, umeshajaa?” Nayo itasema: “Je, hakuna ziada yoyote?”[3]

Vilevile ameeleza kwamba ardhi na mbingu vimesema:

أَتَيْنَا طَائِعِينَ

“Tumekuja hali ya kuwa wenye utiifu.”[4]

Maneno haya yametoka si kupitia njia zake za kawaida. Kadhalika imepokelewa kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alizungumza na mguu[5] aliotiliwa sumu na kwamba jiwe[6] na mti[7] vilimtolea salamu.

[1] al-Bukhaariy (13/453) na al-Adab al-Mufrad (970) na Khalq Af´aal-il-´Ibaad, uk. 131 na Ahmad (3/495). Nzuri kwa mujibu wa al-Mundhiriy katika  ”at-Targhiyb wat-Tarhiyb”. al-Haakim amesema: ”Cheni ni sahihi.” adh-Dhahabiy ameafikiana naye.

[2] al-Bukhaariy (13/453), Abu Daawuud (4738) na Ibn Khuzaymah katika Kitaab-ut-Tawhiyd, uk. 95. Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (1293).

[3] 50:30

[4] 41:11

[5] al-Bukhaariy (6/272).

[6] Muslim (2276).

[7] at-Tirmidhiy (3703).

  • Mhusika: Imaam Swiddiyq Hasan Khaan al-Qanuujiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qatwf-uth-Thamar, uk. 84-85
  • Imechapishwa: 25/05/2019