Aliyepitwa na Dhuhaa kuiswali baada ya Dhuhr

Swali: Je, inafaa kwa mtu aliyepitwa na Dhuhaa kuiswali baada ya Dhuhr?

Jibu: Udhahiri ni kwamba ni Sunnah ambayo pamepita mahali pake. Lakini wakati wa adhuhuri aswali kiasi anachoweza, hata hivyo sio Dhuhaa. Adhuhuri nzima ni wakati wa swalah kama anataka kuswali. Aswali kiasi anachoweza. Sunnah ya Dhuhr umepita wakati wake. Dhuhaa, baada ya jua kuchomoza mpaka kupondoka kwa jua, ni wakati wa kuswali. Vilevile adhuhuri nzima ni wakati wa kuswali mpaka kunaposwaliwa ´Aswr. Vivyo hivyo magharibi na usiku mzima ni wakati wa kuswali.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24533/هل-لمن-فاتته-الضحى-ان-يصليها-بعد-الظهر
  • Imechapishwa: 31/10/2024