Alivyo mzazi, ndivyo anavyokuwa mtoto

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Watu saba watafunikwa na kivuli siku ambayo hakutokuwa na kivuli isipokuwa kivuli Chake; kiongozi mwadilifu, kijana aliyekulia katika kumuabudu Allaah…”

Ni vipi kijana wa leo atakulia katika kumuabudu Allaah?

Jibu: Atakulia kwa hilo akilelewa juu yake na akawa anaishi kwenye nyumba ya ´ibaadah. Hivyo ndivyo mtoto atavyokuwa:

Mtoto wetu amekulia kwa kile ambacho baba yake amemzoweza

Ni jambo lisilokuwa na shaka ya kwamba mtoto hukulia kwa kile ambacho amezowezwa nyumbani. Kheri au shari.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (01) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/muq–14331116.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015