Alipe swawm ya Sunnah baada ya kupata hedhi kwa robo saa kabla ya adhaana?

Swali: Damu ya hedhi ikitoka robo saa kabla ya Maghrib au theluthi saa kabla ya adhaana ilihali nimefunga swawm ya Sunnah ni wajibu kwangu kuilipa?

Jibu: Damu ya hedhi ikimtoka mwanamke aliyefunga, japokuwa ni muda kidogo kabla ya kuzama kwa jua, swawm yake imeharibika. Ikiwa ni swawm ya wajibu basi ni lazima kuilipa. Ikiwa ni swawm ya Sunnah yuko na khiyari; akitaka atailipa na akitaka hatoifunga. Lakini swawm yake juu ya siku hii ni kwa sababu ni siku maalum basi asiifunge.

Kwa mfano mwanamke ana mazowea ya kufunga jumatatu na alkhamisi. Mwishoni mwa siku ya jumatatu kabla ya jua kuzama akajiwa na hedhi. Katika hali hii swawm yake imeharibika. Je, ailipe siku hiyo? Jibu ni kwamba asilipe. Kwa sababu ni swawm iliosuniwa katika siku maalum na imekwishapita. Kwa hivyo ni Sunnah ambayo imekwishapita.

Kwa mfano mwanamke amehisi alama za kupata hedhi lakini hata hivyo haikutoka isipokuwa baada ya kuzama kwa jua kwa dakika tano, je, swawm yake imeharibika? Haikuharibika. Kwa sababu swawm haiharibiki isipokuwa baada ya kutoka kwa hedhi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (67) http://binothaimeen.net/content/1518
  • Imechapishwa: 13/02/2020